NYASA TOURISM FESTIVAL

NYASA TOURISM FESTIVAL

Friday 29 June 2018

KAMPENI YA KUCHANGIA UJENZI WA VYOO BORA MASHULENI

"Tukiwa kwenye kuonyesha mitindo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyoo bora mashuleni kwa ajili ya watoto wa kike, hivyo niliona niwe katika mila na desturi za watu wa nyasa, hapa nikiwa nimebeba jamanda". Mhe. Eng. Stella Manyanya, Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Sunday 10 June 2018

ENG. MANYANYA AONGOZA MKUTANO WA MAWAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI WA AFRIKA YA MASHARIKI

Eng. Stella Manyanya Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji (wa pili kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa Mawaziri wa Afrika Mashariki  wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

SABABU zinazoifanya Nyasa kuwa Benki ya vivutio vya utalii Tanzania

Na Albano Midelo - Songea
...............................................................
WILAYA ya Nyasa mkoani Ruvuma bado ina fursa za maliasili ya kutosha zikiwemo misitu, wanyamapori, samaki, mito, ziwa, fukwe na mali kale ambazo hazijaharibiwa ndiyo maana tunasema wilaya ya Nyasa ni benki ya vivutio vya utalii na uwekezaji.
Moja ya kivutio adimu cha utalii katika wilaya ya Nyasa ni uwepo wa Ziwa Nyasa ambalo ni la tisa kwa ukubwa duniani,ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Ziwa hilo lina kina cha kati ya mita 426 na 758 na hii ni kutokana na kupitiwa na bonde la ufa. Kwa upande wa Tanzania mito mingi inapatikana ikitokea wilaya ya Nyasa katika safu za milima ya Livingstone, mito hiyo ni Ruhuhu, Lumeme, Ruhekei,  Lwika,Mbamba Bay,Likumbo na  Chiwindi ambayo huingiza maji ndani ya Ziwa Nyasa.
Kwa mujibu wa Afisa Maliasili na Utalii wa wilayani Nyasa,ziwa Nyasa ni kuvutio kikubwa cha Utalii kanda ya kusini kwa kuwa limesheheni vitu vingi ndani yake na tabia tofauti ukilinganisha na maziwa mengine ya hapa nchini na duniani kote.
“Baadhi ya tabia za ziwa hili ni uwepo wa maji meupe na maangavu eneo lote la ziwa na mawe marefu ambayo yanajulikana kwa majina ya hiana mala yanayobeba sifa tofauti’’,anasema Bugingo.
Kulingana na ripoti ya utafiti wa mwaka 2011,asilimia 15 ya aina za samaki wa maji baridi duniani wanapatikana ziwa Nyasa ambapo kuna aina ya samaki tofauti zaidi ya 600,huku kukiwa aina ya samaki wa mapambo zaidi ya 400 na viumbe wengine ambao hawapatikani katika ziwa lolote duniani wanapatikana katika maeneo tofauti ndani ya ziwa Nyasa kutegemeana na aina na usalama wa maisha yao.
Jonathan Ruanda Mtaalam wa kuzamia samaki wa mapambo katika ziwa Nyasa na Mfanyabiashara wa samaki hao anasema tangu mwaka 1960 samaki hai wa mapambo toka ziwa Nyasa  walianza kuuzwa katika nchi za Ulaya na Marekani.
Hata hivyo anasema nchi nyingi kama vile Japani, Swedeni, Uturuki, Denmark, Canada, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zilivutiwa na samaki wa mapambo kutoka ziwa Nyasa kutokana na kuwa na sifa ya kipekee yaani rangi nzuri za kupendeza na hakuna sehemu nyingine wanapatikana samaki wa mapambo wa aina hii.Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya anabainisha kuwa Ziwa Nyasa pia limesheheni utajiri mkubwa wa viumbe hai wakiwemo fisimaji, mamba, nyoka na  viboko ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.
“Ndege wanaohamia kutoka Ulaya na baadhi ya nchi za Afrika wanapatikana maeneo ya mwambao mwa ziwa Nyasa ambao ni kivutio kikubwa cha utalii’’,anasisitiza Mhandisi Manyanya.
Manyanya anasema Nyasa imejaliwa utalii wa aina karibu zote ndiyo maana eneo hilo linaitwa ni Benki ya vivutio vya utalii ambavyo bado havijatangazwa kikamilifu ili kuwa moja ya chanzo cha mapato.

Monday 2 January 2017

TAMASHA LA UTALII WILAYA YA NYASA LAVUNJA REKODI

No automatic alt text available.
HATIMAYE tamasha la utalii la aina yake katika Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma limefanyika Mbambabay na Liuli na kuwa gumzo ndani na nje ya nchi baada ya kupata mafanikio makubwa ya kutangaza vivutio lukuki vya utalii vilivyopo katika wilaya hiyo pamoja na fursa muhimu za uwekezaji.

 Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Binilith Mahenge. Tamasha limeshirikisha vyombo vya Habari vya kitaifa na kimataifa lengo likiwa ni kuhakikisha wilaya ya Nyasa inafunguka katika sekta ya Utalii na uwekezaji .

Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa Injinia Stella Mànyanya ndiye alikuwa mwenyeji wa tamasha hilo ambalo limeutangaza Mkoa wa Ruvuma kitaifa na kimataifa.
Image may contain: 3 people, people smiling, people standing and outdoor
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Binilith Mahenge (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tamasha hilo. Wa pili kushoto ni Mwenyeji wa Tamasha hilo, Mhandisi Stella Manyanya ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri, Elimu, Sayansi na Teknolojia.Image may contain: 4 people, people standing, ocean, sky and outdoor
Image may contain: 5 people, people sitting and indoor
Image may contain: 1 person, outdoor
Image may contain: 1 person, shoes and outdoor
Image may contain: one or more people, people standing and outdoor
Image may contain: plant
Samaki wa mapambo Ziwa Nyasa.

Monday 26 December 2016

MBUNGE WA JIMBO LA NYASA AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ENG. STELLA MANYANYA ANAWAKARIBISHA WANANCHI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA UTALII (NYASA TOURISM FESTIVAL)

ZIARA YA NAIBU WAZIRI ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ENG. STELLA MANYANYA VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar baada ya kuhitimisha zaira yake visiwani humo tarehe 20 Desemba, 2016.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akipata vyakula vya Kizanzibari eneo la Forodhani, Zanzibar wakati wa ziara yake.

Thursday 29 September 2016

SAMAKI WA MAPAMBO NYASA NI RASILIMALI ADIMU

Samaki wa mapambo ambao wanapatikana kwa wingi katika eneo la Liuli ziwa Nyasa wanaweza kubadilisha maisha ya wakazi wa mwambao mwa ziwa Nyasa.Inadaiwa samaki mmoja wa mapambo nje ya nchi anauzwa hadi dola za Marekani 500.Leonard Nkomola ni mvuvi wa kuzamia samaki hao tangu mwaka 1993 katika eneo la Liuli,anasema kampuni zimekuwa zinauza samaki hao katika nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,Ufaransa na Norway.Anasema kwa mwaka wana uwezo wa kukamata samaki wa mapambo hadi 10,000.Utafiti umebaini katika eneo la Liuli kuna aina 125 za samaki wa mapambo.Maeneo mengine katika ziwa Nyasa ambako samaki wa mapambo wanapatikana ni Kyela Mkoa wa Mbeya na Ludewa Mkoa wa Njombe.