NYASA TOURISM FESTIVAL

NYASA TOURISM FESTIVAL

Monday 26 December 2016

MBUNGE WA JIMBO LA NYASA AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ENG. STELLA MANYANYA ANAWAKARIBISHA WANANCHI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA UTALII (NYASA TOURISM FESTIVAL)

ZIARA YA NAIBU WAZIRI ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ENG. STELLA MANYANYA VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar baada ya kuhitimisha zaira yake visiwani humo tarehe 20 Desemba, 2016.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akipata vyakula vya Kizanzibari eneo la Forodhani, Zanzibar wakati wa ziara yake.

Thursday 29 September 2016

SAMAKI WA MAPAMBO NYASA NI RASILIMALI ADIMU

Samaki wa mapambo ambao wanapatikana kwa wingi katika eneo la Liuli ziwa Nyasa wanaweza kubadilisha maisha ya wakazi wa mwambao mwa ziwa Nyasa.Inadaiwa samaki mmoja wa mapambo nje ya nchi anauzwa hadi dola za Marekani 500.Leonard Nkomola ni mvuvi wa kuzamia samaki hao tangu mwaka 1993 katika eneo la Liuli,anasema kampuni zimekuwa zinauza samaki hao katika nchi za Ujerumani,Afrika ya Kusini,Ufaransa na Norway.Anasema kwa mwaka wana uwezo wa kukamata samaki wa mapambo hadi 10,000.Utafiti umebaini katika eneo la Liuli kuna aina 125 za samaki wa mapambo.Maeneo mengine katika ziwa Nyasa ambako samaki wa mapambo wanapatikana ni Kyela Mkoa wa Mbeya na Ludewa Mkoa wa Njombe.

FUKWE ZA ZIWA NYASA ZINAONGOZA KWA UBORA

 Fukwe za ziwa Nyasa Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma zinatajwa kuongoza kwa ubora duniani.Zikiendelezwa zinaweza kufungua milango ya utalii katika Wilaya ya Nyasa na Mkoa wa Ruvuma.Hata hivyo jambo la kusitikisha ni kwamba licha ya ubora na upekee wa fukwe hizo kasi ya kuziendeleza katika viwango wa kimataifa ni ndogo.Mataifa mengi duniani hivi sasa yanatoka katika utalii wa kutegemea mbuga za wanyamapori na kuingia katika utalii wa mambo ya kale,fukwe,ngoma na utamaduni hivyo milango ya utalii mwambao mwa ziwa Nyasa ipo wazi.